Sinopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodios
-
Hussein Mohammed ashinda kiti cha urais shirikisho la soka FKF nchini Kenya
07/12/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchaguzi wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF, raundi ya pili ya klabu bingwa Afrika na raga ya wachezaji saba kila upande duniani, fainali za kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa handboli kwa kina dada, debi la Rwanda, mechi za kufuzu ligi ya Afrika basketboli mwaka ujao, droo ya makundi michuano ya klabu bingwa duniani mwaka ujao nchini Marekani mwaka 2026.
-
Fahamu mchezo wa Tong IL Moo Do kuelekea mashindano ya Mombasa Open 2024
30/11/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na washikadau wa mchezo wa Tong IL Moo Do ambao walitutembelea studioni. Mchezo huu unazidi kukua Afrika. Je, unachezwaje, nini umuhimu wake, umepiga hatua kiasi gani, maandalizi ya makala ya Mombasa Open ya mwaka huu yakoje? Pia tumeangazia Ligi ya Klabu bingwa Afrika, msimu mpya wa raga ya HSBC duniani na Kombe la Mataifa ya Afrika ya kina dada mchezo wa handboli ambayo ilianza wiki hii pamoja na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya
-
CAF: Droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada yakamilika
23/11/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada 2024, fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, nini maana ya Tanzania na Uganda kuwakilisha CECAFA kwenye AFCON 2024, mechi za kufuzu ligi ya Afrika ya Basketboli na michuano ya kufuzu Mashindano ya Afrika ya Basketboli, ligi za ukanda na ulaya Pep Guardiola atia saini mkataba mpya klabuni Man City.
-
AFCON 2025: Uganda yafuzu fainali za mwaka kesho huku Kenya, Ghana zikitupwa nje
16/11/2024 Duración: 23minTuliyoyazungumzia ni pamoja na upekee wa klabu ya voliboli nchini Kenya ya Trailblazers, uchaguzi wa FKF nchini Kenya umeanza, mabadiliko ya makocha klabuni Yanga, timu ya taifa ya Kenya ya walemavu ya soka yamaliza nafasi ya nne Kombe la Dunia, uchambuzi wa michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2025 na pigano la Jake Paul dhidi ya Mike Tyson
-
CAF: Ligi ya klabu bingwa barani Afrika 2024 kwa kina dada yaanza nchini Morocco
09/11/2024 Duración: 23minTumeangazia klabu ya Chaux Sport kutoka DRC kubanduliwa kwenye mechi za kufuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024, masaibu ya Yanga SC nchini Tanzania, uchaguzi wa FKF nchini Kenya, mashindano ya kuendesha baiskeli Afrika kwa kina dada nchini Burundi, kifo cha rais wa soka nchini Algeria, matokeo na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya na fainali ya tenisi kwenye mashindano ya WTA
-
Senegal kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki ya kwanza kabisa Afrika, 2026
02/11/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na bodi mpya ya uchaguzi wa shirikisho la soka nchini DRC, waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro abainisha viwanja 20 kwa ajili ya AFCON 2027, timu ya REG nchini Rwanda yafuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024 kwa kina dada, mechi za kufuzu CHAN 2025, hatma ya kocha wa Rwanda Torsten Spittler, Senegal kuandaa michezo ya Olimpiki ya kwanza barani Afrika ya chipukizi mwaka 2026, kocha mpya wa Man Utd, mashindano ya Paris Masters na Brazilian GP Afrika inatarajia michezo ya kwanza ya Olimpiki ya vijana itakayoandaliwa barani Afrika mwaka 2026, jijini Dakar, mji mkuu wa Senegal.Michezo hiyo imepangwa kufanyika kati ya Oktoba 31 na Novemba 13, 2026, tukio ambalo litaleta pamoja wanariadha bora zaidi ulimwenguni kushiriki katika michezo 35 tofauti kwa siku 14.Tamasha la Dakar en Jeux (Dakar in Games) lilipangwa awali kwa kipindi cha Dakar 2022, katika miji mitatu ya mwenyeji wa Dakar, Diamniadio, na Saly.Tangu wakati huo, Dakar en Jeux imekuwa sherehe ya kila mwaka ya michezo na ut
-
Nitawania tena urais wa CAF mwaka 2025, amethibitisha Dkt Patrice Motsepe
26/10/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na taarifa ya Rais wa CAF Patrice Motsepe kuwania tena urais muhula wa pili, hukumu ya CAF katika mechi ya Nigeria dhidi ya Libya, yaliyotukia kwenye ziara ya rais wa Olimpiki ya kimataifa nchini Kenya na Kongamano la tatu la kibiashara la soka Afrika, uchambuzi wa michuano ya Kombe la Dunia la kina dada U17, Senegal ikihifadhi ubingwa wa Afrika soka ya ufukweni, michuano ya ndondi Afrika jijini Kinshasa, PSG kumlipa Mbappe €55M na uchambuzi wa El Clasico leo usiku.
-
Tanzania na Kenya zafuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika U20 mwaka ujao
19/10/2024 Duración: 24minTuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya kufuzu AFCON U20 mwaka ujao, namna timu za Afrika zilicheza kwenye wiki ya kwanza ya Kombe la Dunia la kina dada wasiozidi miaka 17, timu ambazo tayari zimefuzu AFCON ya 2025 nchini Morocco na nafasi ya timu za Afrika Mashariki na Kati, AFCON ya ufukweni yaanza leo nchini Misri, droo ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, mashindano ya magari ya Rwanda Mountain Gorilla Rally, kutimuliwa kwa kocha Kavazovich klabuni Vipers na Ligi za ukanda na Ulaya
-
AFCON U20: DRC yafuzu Kombe La Mataifa Ya Afrika ya mwaka ujao
05/10/2024 Duración: 24minTuliyokuandalia ni pamoja na faniali za kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20, uchambuzi wa vikosi vilivyotajwa na wakufunzi kuelekea raundi ya tatu ya kufuzu AFCON 2025, masaibu ya Samuel Eto'o na kocha wa Senegal Aliou Cisse kutemwa, kifo cha nyota wa basketboli Dikembe Mutombo pamoja na matokeo ya mechi za ligi ya mabingwa ulaya.
-
Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya juu zaidi ya baiskeli barani Afrika
28/09/2024 Duración: 24minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa mechi ya Kombe la Super Cup Afrika, Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya baiskeli Afrika kwa mara ya kwanza, matokeo ya riadha jijini New York, sura mpya za wanariadha watakaoshiriki Berlin Marathon hapo kesho, Ligi za ukanda kwenye soka, voliboli na basketboli lakini pia matokeo ya Kombe la Europa League raundi ya kwanza.
-
CHAN 2024 kuanza Februari 1-28 mwaka 2025 nchini Uganda, Kenya na Tanzania
21/09/2024 Duración: 24minTuliyokuandalia ni pamoja na taarifa ya ziara ya rais wa CAF Patrice Motsepe nchini Kenya, awamu ya pili kufuzu hatua ya makundi mechi za klabu bingwa Afrika, timu za Kenya za soka na mchezo wa Kabaddi tayari kushiriki Kombe la Dunia, timu za taifa Afrika Mashariki zimepanda kwenye msimamo wa dunia wa FIFA, uchambuzi wa raundi ya kwanza mechi za UEFA na mchezo wa ndondi kati ya Anthony Joshua na Daniel Dubois leo usiku.
-
Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei azikwa kwa heshima kamili za kijeshi
14/09/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia hii leo ni mkusanyiko wa uchambuzi na matokeo ya mechi za kufuzu AFCON 2025, mechi za klabu bingwa Afrika kufuzu awamu ya makundi, washindi wa riadha za Diamond League, matokeo ya lLigi ya basketboli ya Afrika U18, droo ya AFCON U20 ukanda wa CECAFA, ligi za ukanda na ulaya pamoja na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya msimu mpya utakaoanza wiki ijayo
-
AFCON 2025: Safari ya kuelekea Morocco yaanza kwa mataifa ya Afrika
07/09/2024 Duración: 24minTuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, kifo cha mwanariadha wa Uganda nchini Kenya, matokeo ya Zurich Diamond League, matokeo ya U18 Afrobasket na Congo Cup, uchambuzi wa matokeo ya mataifa ya Afrika kwenye Olimpiki ya walemavu jijini Paris, mechi za Ligi ya Mataifa ya Ulaya na tuzo za Ballon D'Or mwaka 2024
-
Mashindano ya Tong IL Moo Do, Mombasa Open yafutiliwa mbali kutokana na ufadhili
31/08/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya kufuzu klabu bingwa kwa kina dada, uchambuzi wa vikosi vya timu za Afrika Mashariki na kati kuelekea mechi za kufuzu AFCON 2025, matokeo ya riadha ya Rome Diamond League na riadha za dunia U20, mashindano ya Tong IL Moo Do Mombasa Open kufutiliwa mbali, matokeo ya Olimpiki ya walemavu na uhamisho wa wachezaji ulaya.
-
Mashindano ya kimataifa, Mombasa Open Tong IL Moo Do 2024 yacheleweshwa kwa wiki
24/08/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa mechi za kufuzu klabu bingwa Afrika, riadha za Diamond League, FIBA Afrobasket kwa kina dada, hatma ya mashindano ya Mombasa Open Tong IL Moo Do mwaka huu, unachostahili kujua kuhusu Olimpiki ya walemavu inayoanza wiki ijayo jijini Paris huku kiungo Ilkay Gundogan akirejea klabuni Man City.
-
Namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa kutoka Olimpiki ya Paris
17/08/2024 Duración: 24minJumamosi hii tumezungumzia namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa na mataifa yao kutoka Olimpiki ya Paris, michuano ya klabu bingwa Afrika imeanza kusaka tiketi ya hatua ya makundi, uhamisho tata wa wachezaji wa soka nchini Kenya huku ligi za Afrika Mashariki na Ulaya zikianza kurejea, Mbappe ashinda taji la kwanza Real Madrid, Pochettino kuwa kocha wa Marekani
-
Paris Olimpiki: Tamirat Tola kutoka Ethiopia ndiye mshindi wa mbio za marathon
10/08/2024 Duración: 19minTuliyokuandalia Jumamosi hii kutoka taasisi ya Alliance Francaise, ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya marathon, riadha na mashindano mengine ya Olimpiki ya Paris yaliyotukia wiki hii. Pia tunaangazia fainali kubwa zinazosubiriwa jioni ya leo na kesho asubuhi kwenye marathon ya kina dada lakini pia kifo cha aliyekuwa rais wa tano wa shirikisho la soka Afrika CAF, Issa Hayattou.
-
Jukwaa La Michezo: Fainali ya mita 100 kwa wanaume yasubiriwa, Olimpiki Paris
04/08/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya Olimpiki hapo jana raia wa St Lucia Julien Alfred akishindia taifa lake medali ya kwanza ya Olimpiki, Sudan Kusini yaaga mashindano ya basketboli kibingwa, uchambuzi wa wanariadha wa Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki nusu fainali na fainali kadhaa leo usiku na kesho, uchambuzi wa mechi za nusu fainali ya soka lakini pia kwenye mjadala tunazungumzia kashfa ya jinsia ya mabondia Angela Carini na Imane Khelif
-
Jukwaa La Michezo: Cheptegei aishindia Uganda medali ya kwanza Olimpiki ya Paris
03/08/2024 Duración: 23minJoshua Cheptegei ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 huku Malkia Strikers ikibanduliwa mashindanoni. Morocco na Misri zafuzu nusu fainali huku waafrika kwenye uogeleaji wakifanya vibaya. Pia tutakufahamisha matokeo ya judo, basketboli, kuendesha basikeli na jedwali la medali ambapo Uchina inazidi kuongoza jedwali hilo
-
Paris Olimpiki: Ufaransa yashinda dhahabu ya raga, Kenya ikimaliza nambari tisa
28/07/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya Olimpiki na mjadala kuhusu wanariadha wanaotarajiwa kung'ara kwenye Olimpiki wiki ijayo riadha zitakapoanza pamoja na matokeo ya Toyota Cup Yanga ikiilaza Kaizer Chiefs huku George Russel akishinda mkondo wa Belgian GP kwenye mashindano ya langalanga.