Sinopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodios
-
Olimpiki ya Paris: Mambo muhimu ya kujua kuhusu mashindano ya mwaka huu
20/07/2024 Duración: 17minTuliyokuandalia ni pamoja na mambo muhimu unahitaji kujua kuhusu Olimpiki ya mwaka huu kabla ya kuanza, uchambuzi wa fainali ya CECAFA Kagame Cup kati ya APR ya Rwanda na Red Arrows ya Zambia, tetesi za uhamisho Afrika Mashariki n aUlaya pamoja na matokeo ya Tour de France ikielekea ukingoni huku kocha wa Uingereza Gareth Southgate akijiuzulu kuifunza timu ya taifa ya wanaume.
-
Timu ya Kenya yaanza kuwasili Miramas, Ufaransa tayari kwa Olimpiki
13/07/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na droo ya hatua ya awali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao, matokeo ya Monaco Diamond League, Team Kenya yaanza kuwasili Ufaransa tayari kwa Olimpiki, matokeo ya CECAFA Kagame Cup na tetes iza uhamisho pamoja na uchambuzi wa fainali ya EURO, Copa America na fainali za tenisi kwenye Wimbledon.
-
Shirikisho la soka barani Afrika CAF latangaza droo ya michuano ya kufuzu AFCON 2025
06/07/2024 Duración: 23minMiongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya mwaka 2025, fainali ya Cosafa Cup, mipango ya Team Kenya kuelekea Olimpiki ya mwaka huu, uchambuzi wa mechi za robo fainali michuano ya Euro na Copa America, raia wa Eritrea Girmay Hailu Biniam ashinda hatua ya nane ya Tour de France wakati kocha wa Manchester United Erik ten Hag aongeza mkataba wake.
-
CAF: Kenya Police FC yafuzu kushiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao
29/06/2024 Duración: 23minTumekuandalia mengi ikiwemo matokeo na uchambuzi wa mashindano ya COSAFA Cup inayoendelea nchini Afrika Kusini, Leopards voliboli ya ufukweni yafuzu Kombe la Dunia wakati Kinshasa yajiandaa kuandaa mechi za kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa basketboli ya kutumia viti vya magurudumu, Kenya yateua kikosi kitakachoshiriki riadha za dunia U20 nchini Peru, tetesi za uhamisho katika vilabu vya Afrika Mashariki, Kenya Police yafuzu kombe la shirikisho barani Afrika msimu ujao. Tour de France yaanza leo nchini Italia kabla ya kurejea Ufaransa huku michuano ya EURO na Copa America ikiingia hatua za mtoano.