Sinopsis
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
Episodios
-
Historia ya Kenya kupata Uhuru pamoja na Maonyesho ya Sanaa ya Uchoraji Alliance Francaise Nairobi
15/12/2024 Duración: 19minMakala haya yataangazia Historia ya nchi ya Kenya na jinsi ilivyopata Uhuru,kwenye kipengele cha pili utaskia safari ya vijana wanaofanya sanaa ya Uchoraji kutoka shirika lisilo la kiserikali la Uweza Art Gallery na mwisho kabisa kwenye kipengele cha historia ya mwanamuziki utaskia historia yake Juma Jux kutokea Tanzania.
-
Teknolojia yabadilisha muziki ,Ujio wake Msanii Sean Paul nchini Kenya
08/12/2024 Duración: 19minTutaangazia historia ya muziki wa Afrika, tukiangalia mabadiliko makubwa yaliyotokea kabla na baada ya kuibuka kwa teknolojia. Muziki wa Afrika ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu, na umetumika kwa karne nyingi kama njia ya kuwasiliana, kusherehekea, na kuponya.
-
Hatuwa za mwisho za maandalizi ya tamasha la watu wa kabila la bashi la desemba 6
01/12/2024 Duración: 20minUhusiano baina ya lugha na utamaduni, mila na mirathi ya jamii kwa jumla huenda ukafahamika angalau kwa wepesi, iwapo tutazingatia mambo kadhaa ikiwemo lugha na matumizi yake, tabia, utu, utamaduni, mila,mitindo na mengineo. Watu wa kabila la washi mashariki mwa DRC wameandaa tamasha la kutambulisha utamaduni wao, ambalo ni msimu wa pili na limepangwa kufanyika desemba 6 hadi 8 huko Bukavu. Katika makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anakuletea sehemu hii ya tatu na ya mwisho ya maandilizi ya makala haya. unaweza kusikiliza sehemu ya kwanza kubonyeza hapa (sehemu ya kwanza) Lakini pia sehemu ya pili kwa kubonyeza hapa (Sehemu ya pili) Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako asiependa makuu unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali
-
Msani Olivier kutoka Bukavu azungumzia tamasha la watu wa kabila la washi Nov 24 2024
23/11/2024 Duración: 19minMakala haya Ali Bilali anazungumza na msanii Oliver wa nyimbo za asili ya washi wahavu mashariki mwa DRC kuelekea tamasha la Bushi ama Festival de Bushi. Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako asiependa makuu unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali
-
Maandalizi ya Tamasha la watu wa Kabila la Washi kutoka Bukavu sehemu ya kwanza.
18/11/2024 Duración: 20min -
Shindano la filamu kwa kutumia simu ya Mkononi na msanii kutoka Mombasa Rojo Mo
09/11/2024 Duración: 19minKaribu katika makala changu chako chako changu Jumapili yaleo ambapo tutakijita zaidi kwenye matokeo ya shindano la kutengeneza filamu kwa kutumia simu ya mkononi liliooandaliwa na Alliance Francaise ya Nairobi nchini Kenya na kwenye Muziki tutakuwa naye msanii kutoka Mombasa Rojo Mo. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu, restons ensemble mwanzo hadi tamati, yaani tubaki pamoja mwanzo hadi mwisho.
-
Alliance Francaise ya Nairobi inavyoikuza sanaa ya uigizaji jukwaani sehemu ya kwanza.
04/11/2024 Duración: 19minKatika Makala haya Ali Bilali amejielekeza Alliance Francaise ya Nairobi ambayo imeandaa Onyesho la Kwanza la tamthilia ya ‘Mgonjwa Mwitu’, utayarishaji wao wa kila mwaka wa maigizo yaliyotolewa na tamthilia za waandishi mashuhuri wa Ufaransa. Kwa maadhimisho ya miaka 75, chaguo ni 'Le Malade Imaginaire' na Molière. Hii ni comedy ya mwisho kuandikwa na Molière. Ingawa ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mnamo 1673, kichekesho hiki cha kejeli, mojawapo ya bora zaidi za Moliere, hakijapoteza mvuto wake wa dhati na wa ulimwengu wote.Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako @billy_bilali kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali
-
Fahamu hapa kuhusu liliokuwa soko la watumwa nchini DRC Oct 20 2024
04/11/2024 Duración: 20minKaribu katika Makala Changu Chako Chako Changu, ambapo Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu ameungana na Denise Maheho kutoka Lubumbashi kuzungumzia kuhusu iliokuwa barabara ya watumwa zama za ukoloni.Kumbuka pia kutuachia comment na kumfollow mtangazaji wako asiependa makuu @billy_Bilali kwenye mitandao yake ya kijamii Instagram na facebook.
-
Utamaduni wa ndoa kulingana na kabila la Wameru sehemu ya pili Oct 13 2024
13/10/2024 Duración: 20minAli Bilali ndio jina langu tunakutana tena Jumapili hii katika makala Changu Chako Chako Changu ambapo nakuletea sehemu ya pili ya Makala kuhusu Utamaduni w andoa kulingana na kabila la Wameru, kwenye le parler francophone nitakupa ratiba ya shughuli kwenye vituo vya Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamaliza na kibao Pambe chake Christian Bella kutoka huko nchini Tanzania, Karibu ama Bienvenue.
-
Utamaduni wa watu wa Kabila la Wameru kutoka nchini Kenya
06/10/2024 Duración: 19minMakala haya mtangazaji wako Ali Bilali anazungumzia kuhusu utamaduni wa watu wa kabila la Wameru kutoka nchini Kenya, wapo pia nchini Tanzania.
-
Utamaduni wa ndoa kabila la wamakonde na wahangaza kutoka nchini Tanzania sehemu ya 2
29/09/2024 Duración: 20minkaribu, Jumapili nyingine kuwa nami katika Makala Changu Chako Chako Changu Makala ambayo hukuletea Historia na utamaduni wa mambo mbalimbali, le Parler francophone na Muziki. Wiki iliopita nilikuletea Utamaduni wa ndoa kutoka makabila ya Wamakonde na wahangaza, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili. Na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba za shughuli za kitamaduni kutoka Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam, Tutamaliza na Wimbo wa Ibrah kutokz Tanzania
-
Utamaduni wa watu wa makabila ya wahangaza na wamakonde kutoka nchini Tanzania
22/09/2024 Duración: 20minKatika makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Amua Rushita kutoka Mkoa wa Mtwara pamoja na Hillary Alexanda Ruhundwa kutoka Mkoa wa Ngara nchini Tanzania kuzungumzia utamaduni wa ndoa kulingana na makabila hayo mawili. Kumbuka pia nawe unaweza kushiriki moja kwa moja studio au kwa njia ya simu. Wasiliana na mtangazaji wako asiependa makuu kufahamu zaidi.
-
Toleo la 11 la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon kutolewa huko Benin
26/08/2024 Duración: 19minRFI inaandaa toleo la kumi na moja la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon, kwa heshima kwa waandishi wake wawili waliouawa kaskazini mwa Mali Novemba 2, 2013. Bourse hii, ambayo huwafunza waandishi wa habari vijana kumi wa redio na mafundi vijana kumi wa kuripoti kila mwaka, iko wazi. kwa wagombea kutoka nchi zote za Afrika zinazozungumza Kifaransa. Mafunzo hayo yatafanyika Cotonou. Maombi yamefunguliwa hadi Jumapili Agosti 25 saa sita usiku saa za Paris.
-
Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa mahari kwa baadhi ya makabila barani Afrika
26/08/2024 Duración: 19minMakala haya yanaangazia kuhusu gharama ya sherehe za harusi katika karne hii, hususan ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kufanaikisha sherehe.
-
Changu chako chako changu Tasnia ya ulimbwende sehemu ya pili
13/08/2024 Duración: 20minKaribu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu Ulimbwende au Model,
-
Changu Chako Chako Changu tasnia ya ulimbwende sehemu ya kwanza Agost 04 2024
04/08/2024 Duración: 20minKaribu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea mambo mbalimbali ya utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sanaa ya Ulimbwende au Model, na kwenye la parler francophone nitakuletea shughuli zinazoendelea kwenye vituo vya Alliance francaise za ukanda kipindi hiki cha michuano ya Olympiki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue.
-
Historia ya kabila la Wabukusu pamoja na sanaa ya muziki kutokea kwa Bendi ya An Noor
21/07/2024 Duración: 20minKaribu kwenye makala ya changu chako ,chako changu juma hili ukiwa nami Florence Kiwuwa. Na kwenye kipengele cha historia hii leo tutaangazia historia ya kabila la Waluhya wanaofahamika kama wabukusu kisha kwenye kipengele chetu cha pili cha LeParle Francophone tutaangazia maonyesho ya Taarab yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance France kisha tutamalizia na mwanamuziki wa Kenya almarufu kama Freshely Mwamburi.
-
Matumizi ya lugha ya kiswahili katika enzi ya Kijiditali
16/07/2024 Duración: 20minKiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 afrika mashariki na kwenye makala haya ya changu chako,chako changu ,Florence Kiwuwa amefanya majadiliano na wanafunzi katika chuo kikuu cha Multmedia ili kujua kuhusu mchango wa lugha hii katika kuendeleza utamaduni na utengamano na vilevile katika kipengele cha muziki amemuangazia mwanamuziki wa Tanzania Harmonize.
-
Changu Chako Chako Changu maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 14 ya RFI Kiswahili
07/07/2024 Duración: 19minKaribu katika Makala Changu Chako Chako Changu jumapili ya leo ambapo nakulrtea Makala maalum kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 14 tangu Ple RFI Kiswahili ilipoanza kupeperusha matangazo yake mubashara kutoka nchini Tanzania ambapo ilikuwa idhaa ya kwanza ya Kimataifa kutangaza ikiwa Afrika mashariki. Na kwenye Muziki nitakuletea Burudani ya Muziki wa Idd Aziz Kiswahili kitukuzwe wakati huu tukielekea kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani. Mimi naitwa Ali Bilali, Bienvenue ama Karibu. Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako Ali Bilali kwa kubonyeza hapa @billy_bilali
-
Changu Chako Chako Changu, maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa DRC
06/07/2024 Duración: 20minMakala haya Ali Bilali anazungumzia kuhsu maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru wa DRC.