Learning By Ear Elimu Ya Jamii

Informações:

Sinopsis

Kupitia vipindi vyetu tunajaribu kuwahamasisha vijana wa Afrika kuhusu elimu ya jamii. Inasaidia kuyafanya maisha yao kuwa rahisi.

Episodios

 • Ardhi ya Ahadi – Hadithi ya Uhamiaji wa Waafrika barani Ulaya

  Ardhi ya Ahadi – Hadithi ya Uhamiaji wa Waafrika barani Ulaya

  12/08/2013 Duración: 11min

  Huku Farahani na Sule wakiota kuwa na maisha bora Ulaya, mwanafunzi Linda tayari yuko njiani kuelekea huko. Mchezo huu unalinganisha ndoto za vijana wa Kiafrika za kusoma na kufanya kazi Ulaya na hali halisi ya mambo.

 • Haki za binaadamu ni za watu wote lakini...

  Haki za binaadamu ni za watu wote lakini...

  06/08/2013 Duración: 12min

  Kila binaadamu hapa duniani ana haki ya uhuru na usawa - kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binaadamu. Lakini katika mataifa mengi barani Afrika, utakuta haki hizi zinaendelea kukanyagwa na kukiukwa.

 • Kazi –Kipindi 8 – Mwanamuziki

  Kazi –Kipindi 8 – Mwanamuziki

  16/03/2011 Duración: 10min

  Katika kipindi hiki, tutageuka na kuangazia sekta ya muziki na kupata nafasi ya kumfahamu Chimere Emejuobi, mwimbaji kutoka Lagos. Muziki ni muhimu sana katika jamii nchini Nigeria.

 • Kazi – Kipindi 7 – Vijana wasio na ajira

  Kazi – Kipindi 7 – Vijana wasio na ajira

  16/03/2011 Duración: 10min

  Hatutazungumzia juu ya taaluma fulani, lakini ni juu ya wale wote ambao hawana ajira. Idadi ya wasio na ajira hususan miongoni mwa vijana imeongezeka sana barani Afrika. Kila kijana mmoja kati ya watano hana ajira.

 • Kazi – Kipindi 6 – Kazi za sekta isiyorasmi

  Kazi – Kipindi 6 – Kazi za sekta isiyorasmi

  16/03/2011 Duración: 10min

  Katika mji mkuu wa Kenya, tunakutana na watu wanaofanya shughuli zao ambazo ziko nje ya sekta rasmi ya uchumi. Wanashughulika kinyume na sheria bila ya kuwa na elimu stahiki, mfano biashara ya kiwango cha rejareja.

 • Kazi – Kipindi 5 – Mwalimu

  Kazi – Kipindi 5 – Mwalimu

  16/03/2011 Duración: 10min

  Tutaiangazia sekta ya elimu huko Lagos Nigeria. Kwa jumla waalimu hulipwa mshahara mdogo. Lakini kwa baadhi yao, la muhimu ni hamasa ya kufundisha na hamu ya kuwapatia ufahamu wanafunzi wao.

 • Kazi – Kipindi 4 – Meneja wa Hoteli

  Kazi – Kipindi 4 – Meneja wa Hoteli

  16/03/2011 Duración: 10min

  Katika kipindi hiki tutapata nafasi ya kumfahamu kijana mmoja nchini Uganda ambaye ni meneja wa hoteli. Je kuna ugumu gani wa kufanya kazi ya umeneja wa hoteli katika nchi zinazoendelea kama Uganda?

 • Kazi – Kipindi 3 –Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari

  Kazi – Kipindi 3 –Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari

  16/03/2011 Duración: 10min

  Mtandao wa Intaneti ni lango kuu la kujiunga na jamii duniani. Hata hivyo bado watu wengi hawana uwezo wa kuitumia. Wafanyakazi katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wanajaribu kulibadilisha suala hili.

 • Kazi –Kipindi 2 – Fundi magari

  Kazi –Kipindi 2 – Fundi magari

  16/03/2011 Duración: 10min

  Kuna taaluma ambazo zinachukuliwa kuwa ni za wanaume tu. Ni wanawake wangapi wanaoweza kurekebisha magari au pikipiki? Estelle Christian Ouedraogo, kutoka Burkina Faso, ni miongoni mwao. Tujiunge naye!

 • Kazi – Kipindi 1 – Nesi

  Kazi – Kipindi 1 – Nesi

  16/03/2011 Duración: 09min

  Katika mfulululizo huu, tutakutambulisha kwa vijana wa kiafrika wenye taaluma mbalimbali, na kukupatia undani wa shughuli zao. Kwanza tutapata nafasi ya kumfahamu Judith ambaye ni nesi katika hospitali huko nchini Kenya.

 • Ngano za Afrika – Kipindi 10 – Tumbiri na Kobe

  Ngano za Afrika – Kipindi 10 – Tumbiri na Kobe

  16/03/2011 Duración: 11min

  “Wanaopata, wanaoweka. Anayepata kitu fulani njiani anaruhusiwa kukimiliki” Je, ni rahisi namna hiyo kila mara? Sikiliza hadithi ya kobe na tumbiri mjanja aliyelazimika kupata adhabu kuokoa mkia wake!

 • Ngano za Afrika – Kipindi 09 – Mrembo kuliko wote

  Ngano za Afrika – Kipindi 09 – Mrembo kuliko wote

  16/03/2011 Duración: 10min

  Hadithi yetu inatokea zamani za kale, wakati tausi alipokuwa angali mweupe. Jifunze jinsi alivyopata rangi zake nyingi na wakati huo huo kuiharibu sauti yake

 • Ngano za Afrika – Kipindi 08 – Bundi na Nyenje

  Ngano za Afrika – Kipindi 08 – Bundi na Nyenje

  16/03/2011 Duración: 12min

  Siku moja bundi mzee na nyenje kijana wanakuwa majirani. Mwanzoni wanafurahia kuishi kwa pamoja, lakini kadri muda unavyopita bundi anakasirika na nyenje anavunjika moyo. Watafanya nini?

 • Ngano za Afrika – Kipindi 07 – Dikum Dakum

  Ngano za Afrika – Kipindi 07 – Dikum Dakum

  16/03/2011 Duración: 12min

  Katika hadithi hii, marafiki zetu wanyama wenye njaa wanalazimika kutafuta njia ya kuchuma matunda mtini. Inaonekana kuwa kazi rahisi lakini mti wa maajabu wa marula unawafunza somo zuri

 • Ngano za Afrika – Kipindi 06 – Mfalme asiye na Ufalme

  Ngano za Afrika – Kipindi 06 – Mfalme asiye na Ufalme

  16/03/2011 Duración: 12min

  Mwanamke kizee akamwambia Amadou. “Usijiingize katika hali usizoweza kukabiliana nazo! Fuata maagizo yangu.” Lakini wakati mwingine inahitaji uhodari mkubwa mtu kukubali udhaifu wake, kama Amadou atakavyogundua

 • Ngano za Afrika – Kipindi 05 – Kassi na Kaloo

  Ngano za Afrika – Kipindi 05 – Kassi na Kaloo

  16/03/2011 Duración: 10min

  Kassi na Kaloo – marafiki wasioweza kutenganishwa! Angalau hali ilikuwa hivyo kabla farasi hao wawili wa kupendeza kupandwa na wafalme wawili mahasimu. Watafanya nini wakati vita vitakapozuka kati ya falme zinazopigana?

 • Ngano za Afrika – Kipindi 04 – Fisi, Nyoka, Chui na Ngiri

  Ngano za Afrika – Kipindi 04 – Fisi, Nyoka, Chui na Ngiri

  16/03/2011 Duración: 11min

  Je unaamini hirizi za bahati na mawe ya mazingaombwe? Sawa, zuia wazo hilo na tumruhusu ngiri atueleze hadithi yake kuhusu kilichomuokoa, na vipi

 • Ngano za Afrika – Kipindi 03 – Lipua Lipua

  Ngano za Afrika – Kipindi 03 – Lipua Lipua

  16/03/2011 Duración: 12min

  Fuata nyayo za Lipua! Njiwa jasiri ana kibarua cha umuhimu mkubwa. Je Lipua atamshinda mfalme mlafi na muovu Karamba na kuwaokoa ndege wenzake wasife kutokana na njaa?

 • Ngano za Afrika – Kipindi 02 – Simba, Fisi na Tai

  Ngano za Afrika – Kipindi 02 – Simba, Fisi na Tai

  16/03/2011 Duración: 09min

  Zamani paliondokea simba na fisi mwenye njaa. Kilichoanza kama uhusiano wa ajabu lakini wa furaha, kinamalizika huku fisi akiwa amejeruhiwa maisha yake yote na tai akipoteza manyoya yake kadhaa

 • Ngano za Afrika – Kipindi 01 – Masaibu ya Chura Mbott

  Ngano za Afrika – Kipindi 01 – Masaibu ya Chura Mbott

  16/03/2011 Duración: 12min

  Katika mfululizo mwingine wa kusisimua, tunautembelea ulimwengu wa mjusi kafiri Sindakh na chura aitwaye Mbott – hadithi kuhusu urafiki, uaminifu na usaliti

página 1 de 3