Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Rais Ruto avunja baraza la mawaziri, uchaguzi huko Rwanda, usalama wazorota DRC
13/07/2024 Duración: 20minMakala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.
-
DRC: Wanajeshi wanaodaiwa kutoroka adui kwenye mapambano wahukumiwa
06/07/2024 Duración: 20minMiongoni mwa yale utakayosikia katika makala ya wiki hii ni pamoja na hatua ya Rais wa Kenya William Ruto kuzungumza na wapiga kura kwa njia ya mtandao wa X, wanajeshi waliotoroka adui DRC kuhukumiwa na vilevile mkutano wa nchi za Sahel zinazoongozwa na wanajeshi.
-
Ruto asema hatasaini mswada wa fedha 2024, M23 wauteka mji wa Kanyabayonga
29/06/2024 Duración: 20minMakala hii imeangazia maandamano nchini Kenya huku rais Ruto akisema hatasaini mswada wa fedha wa 2024 uliokuwa umeidhinishwa na wabunge walio wengi, waasi wa M23 huko DRC walifanikiwa kuuteka mji wa kimkakati wa Kanyabayonga wilayani Lubero mashariki mwa DRC, mgomo wa wafanyabiashara nchini Tanzania, na nini hatima yake, siasa za Afrika kusini lakini pia mdahalo kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na Joe Biden kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, yaliyojiri nchini Ufaransa na kwengineko Duniani.
-
Maandamano nchini Kenya kupinga mswada wa fedha 2024, hali ya usalama DRC
22/06/2024 Duración: 20minMakala imeangazia hatua ya wabunge wa Kenya kuidhinisha mswada wa fedha wa 2024 kuingia katika hatua ya pili kabla ya kupitishwa licha ya maandamano makubwa nchini, ziara ya rais Felix Tshisekedi huko Lubumbashi, na kuendelea kwa mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23, Uganda yawasamehe waasi wa zamani wa ADF, kuapishwa kwa rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, hali huko Afrika Magharibi, na kwengineko duniani