Habari Za Un

UN: Hali Rafah ni mbayá mashambulizi yanakatili maisha na kufurusha watu kwa maelfu

Informações:

Sinopsis

Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Kwa mujibu wa tarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kuendelea kwa mashambulizi ya wanajeshi wa Israel, kwenye Ukanda wa Gaza kwa njia ya angani, ardhini na baharini kunazidisha vifo vya raia, kulazimika wengi kukimbia na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya makazi na miundombinu mingine muhimu ya raia. Shirika hilo limeongeza kuwa na mashambulizi ya ardhini ya Israeli yanaendelea kupanua wigo, haswa katika maeneo ya kusini mwa mji wa Gaza na Mashariki mwa Rafah, hususan karibu na Kerem Shalom na vivuko vya Rafah.Kana kwamba hayo hayatoshi Philippe Lazzarini ambaye ni Kamishina Mkuu wa UNRWA amesema kumekuwa na jaribio lingine la uchomaji moto la watoto na vijana wa Israel kwenye majengo ya UNRWA huko Jerusalem jana usiku. A