Noa Bongo Uchumi Na Mazingira

Informações:

Sinopsis

Katika mfululizo wa vipindi vyetu utapata fursa ya kujifunza kuhusu masuala ya uchumi na biashara pamoja na mazingira.

Episodios

 • Mti unapoanguka… - Kukatwa kwa misitu barani Afrika

  Mti unapoanguka… - Kukatwa kwa misitu barani Afrika

  13/03/2014 Duración: 12min

  Afrika ina kiwango kikubwa cha ukataji misitu kuliko mabara mengine yote duniani. Hili lina athari kubwa kwa maisha ya Waafrika kama hawa katika mchezo wetu wanaoishi katika kambi ya wakimbizi baada ya vita vya kikatili.

 • Anasa ya Kuazima – Hatari ya Kuchukua Mkopo

  Anasa ya Kuazima – Hatari ya Kuchukua Mkopo

  06/08/2013 Duración: 11min

  Tatizo linaanzia na ari ya kutaka kumiliki baiskeli mpya ya kifahari. JD hana fedha za kutosha lakini anashindwa kuvumilia na kuchukua mkopo – ingawa hajui atakavyoulipa mkopo huo. Je, somo hili litamuathiri vipi JD?

 • Ufisadi - Tembo chumbani

  Ufisadi - Tembo chumbani

  06/08/2013 Duración: 11min

  Iwe shuleni, kazini au hata barabarani, familia ya Odhiambo inajikuta ikishinikizwa na athari za ufisadi licha ya juhudi za kutaka kuishi maisha huru yasiyo na dosari ya uovu huu. Watawezaje kuepukana na vitendo hivyo?

 • Wajasirimali wa kiafrika – Wenye mafanikio na wenye kuwajibika

  Wajasirimali wa kiafrika – Wenye mafanikio na wenye kuwajibika

  10/05/2012 Duración: 11min

  Hulala kidogo sana, hawafahamu neno „starehe“ lakini wanaipenda kazi yao na wanajitoa kwa jamii wanamoishi. Hili ni jambo linalowaunganisha wafanyabiashara wote wa Kiafrika tunaowatambulisha katika mfululizo wetu mpya.

 • Utandawazi - Rafiki na adui wa Afrika

  Utandawazi - Rafiki na adui wa Afrika

  25/05/2011 Duración: 09min

  Vipindi vya Noa Bongo vinachunguza kwa kina athari za utandawazi barani Afrika. Kupitia vipindi vyetu wasikilizaji wanaweza kukutana na watu wanaochangia kuufanikisha utandawazi na wale wanaoathiriwa na utandawazi.

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 10 – Habari nzuri sana

  Uhamiaji mijini – Kipindi 10 – Habari nzuri sana

  16/03/2011 Duración: 11min

  Katika awamu ya mwisho ya safari, tunaona mabadiliko katika hadithi wakati Tingo anapoonyesha nia ya dhati katika chama. Baki na Zeina wanapatana kwa kinywaji. Tujiunge nao!

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 09 – Fikra zilizogubikwa na wingu jeusi

  Uhamiaji mijini – Kipindi 09 – Fikra zilizogubikwa na wingu jeusi

  16/03/2011 Duración: 12min

  Tingo hafurahii ufanisi wa chama na huenda akawa na njama fulani. Hii itakuwa na maana gani kwa mashujaa wetu?

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 08 – Furaha ya mapenzi

  Uhamiaji mijini – Kipindi 08 – Furaha ya mapenzi

  16/03/2011 Duración: 12min

  Hadari amebadili nia na Baki amebadili mipango – hatua inayomfurahisha sana Zeina. Tufuatilie mabadiliko yote yanayoendelea.

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 07 – Kushindwa kwa rushwa

  Uhamiaji mijini – Kipindi 07 – Kushindwa kwa rushwa

  16/03/2011 Duración: 12min

  Katika kipindi hiki Baki anapelekwa hospitalini – nini kilichotokea? Lakini kwanza tutafute jinsi chama kinavyoendelea na vipi mashujaa wetu chipukizi wanavyokabiliana na changamoto.

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 06 – Kukabiliwa na vikwazo huku ukiniwa na shinikizo

  Uhamiaji mijini – Kipindi 06 – Kukabiliwa na vikwazo huku ukiniwa na shinikizo

  16/03/2011 Duración: 12min

  Kwa nini Ben anakataa pendekezo zuri kutoka kwa Tingo, ingawa chama kinahitaji fedha? Kipindi kinapofikia tamati, kitu kingine kinaendelea kati ya Ben na Nana.

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 05 – Umuhimu gani wa kuwa sahihi iwapo uko peke yako

  Uhamiaji mijini – Kipindi 05 – Umuhimu gani wa kuwa sahihi iwapo uko peke yako

  16/03/2011 Duración: 12min

  Mpaka sasa kila kitu kinaonekana kwenda kulingana na mpango. Wanakijiji wanauonaje mradi huo? Tunaungana na mashujaa watatu katika mkutano na Hadari na tusikilize huku wakifanya mkutano wao wa kwanza wa mwaka.

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 04 – Ndoto ya kila mwanamke

  Uhamiaji mijini – Kipindi 04 – Ndoto ya kila mwanamke

  16/03/2011 Duración: 12min

  Hatua kwa hatua, marafiki zetu wanapiga hatua wanapojaribu na kuungwa mkono na wanakijiji. Hata hivyo uhusiano kati ya Baki na Zeina unaonekana ukichukua mkondo tofauti.

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 02 – Kuwa na majukumu uhamishoni

  Uhamiaji mijini – Kipindi 02 – Kuwa na majukumu uhamishoni

  16/03/2011 Duración: 12min

  Ungana na marafiki zetu wanapofikiria kuvumbua mpango wa biashara kwa chama chao cha kilimo. Lakini Baki ana jambo lengine akilini mwake.

 • Uhamiaji mijini – Kipindi 03 – Kipato cha kila siku

  Uhamiaji mijini – Kipindi 03 – Kipato cha kila siku

  16/03/2011 Duración: 12min

  Baki, Zeina na Ben wanataka kuanza kwa ufanisi. Kwa bahati mbaya kurejea kijijini huenda kusiwe rahisi kama inavyoonekana na si kila mtu anafurahia kuwaona.

 • Uhamiaji mijini– Kipindi 01 –Bila kazi mjini hakufai

  Uhamiaji mijini– Kipindi 01 –Bila kazi mjini hakufai

  16/03/2011 Duración: 12min

  Katika vipindi hivi vipya, Ben, Baki na Zeina watatueleza matukio yasiyo ya kawaida wanapoamua kuondoka mjini kwenda kijijini kutimiza ndoto zao.

 • Mazingira Afrika – Kipindi 10 – Vyakula vya baharini

  Mazingira Afrika – Kipindi 10 – Vyakula vya baharini

  16/03/2011 Duración: 09min

  Kwa nini ni muhimu kuwafundisha wavuvi kutumia nyavu ili kuwalinda kaa? Juhudi gani zinaweza kuchukuliwa kuwalinda Papa? Sikiliza na ufahamu zaidi juu ya hilo na mengine.

 • Mazingira Afrika – Kipindi 9 – Uvuvi wenye madhara

  Mazingira Afrika – Kipindi 9 – Uvuvi wenye madhara

  16/03/2011 Duración: 09min

  Kipindi hiki kinazungumzia uvuvi wa kutumia baruti unavyoathiri matumbawe ambayo yanahitaji karne kujengeka, lakini yanaweza kuharibiwa kwa sekunde moja tu. Nini kinachowakumba wanyama na mimea ya baharini?

 • Mazingira Afrika – Kipindi 8 – Jangwa

  Mazingira Afrika – Kipindi 8 – Jangwa

  16/03/2011 Duración: 09min

  Majangwa barani Afrika yamekuwa yakiongezeka. Hii ni kutokana na shughuli za kibinaadamu duniani kwa mfano ongezeko la malisho pamoja na ukataji miti. Je, ni jinsi gani wakulima wanawajibika kwa hali hiyo?

 • Mazingira Afrika – Kipindi 7 – Ukataji miti

  Mazingira Afrika – Kipindi 7 – Ukataji miti

  16/03/2011 Duración: 09min

  Ukataji miti umesababisha madhara makubwa kwa mazingira. Bara la Afrika limepoteza misitu mingi kuliko bara lingine lolote. Fahamu kuhusiana na biashara haramu ya mbao pamoja na madhara yake.

 • Mazingira Afrika – Kipindi 6 –Nishati Endelevu

  Mazingira Afrika – Kipindi 6 –Nishati Endelevu

  16/03/2011 Duración: 09min

  Mahitaji ya mafuta, mkaa na gesi bado ni makubwa. Lakini vyanzo vya nishati hii si vya kudumu, kwa hivyo tutapata wapi nishati hii? Tutaangazia nishati nyingine mbadala na inayoweza kutumika tena kama vile upepo na jua.

página 1 de 2